Wednesday, 26 March 2014

WARIOBA AFUGUKA



 
Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta (kulia) akiongoza kikao cha kwanza cha Kamati ya Uongozi ya Bunge hilo, mjini Dodoma jana.  
 
Dar es Salaam. Wakati Ikulu ikitangaza kwamba Rais Jakaya Kikwete amevunja Tume ya Mabadiliko ya Katiba, tume hiyo imetoa ufafanuzi wa baadhi ya maeneo ya Rasimu ya Katiba.
Taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana, ilieleza kuwa Tume ya Jaji Joseph Warioba ilivunjwa tangu Machi 19, ikiwa ni siku moja baada ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba bungeni mjini Dodoma.
Wakati taarifa ya Tume ya Warioba ilitolewa jana jioni, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilikuwa imeshatoa taarifa ya kuvunja tume hiyo mapema jana ikieleza kuwa shughuli za tume hiyo zilikoma tangu  Jumatano iliyopita.
“Kwa mujibu wa kifungu cha 31 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano alivunja rasmi Tume ya Mabadiliko ya Katiba tarehe 19 Machi, 2014 kwa Tangazo la Serikali Na.81 la tarehe 21 Machi, 2014,” ilisema taarifa hiyo ya Ikulu.
Hata hivyo,  Jaji  Warioba aliliambia gazeti hili jana kuwa hadi wanakutana juzi kwenye kikao cha mwisho cha tathmini walikuwa hawajapokea barua ya kuvunjwa kwa tume yake.
“Barua ya Ikulu tumeipokea leo. Tulikuwa hatuna taarifa kwamba tume yetu imevunjwa hadi tulipopokea barua leo (jana). Tulifanya kikao chetu cha mwisho cha tathmini jana (juzi),”  alisema Warioba alipozungumza na Mwananchi jana jioni.
Warioba pia alithibitisha kwamba taarifa ya ufafanuzi (imechapishwa ukurasa wa 37) ni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
<MWANANCHI>

No comments:

Post a Comment