Ndege ya MH370 ya Malaysia ilibadili mkondo

Ndege ya Malaysia iliyotoweka
Mkuu
wa jeshi la anga la Malaysia, amekanusha madai kuwa ndege ya Malaysia
iliyotoweka, ilionekana mara ya mwisho Magharibi ya rasi ya nchi hiyo,
eneo ambalo ni mbali zaidi na njia iliyostahili kupita.
Generali
Rodzali Daud, amesema kuwa hawawezi kupuuza uwezekano huo, lakini
amesema madai kuwa mawasiliano ya ndege hiyo yalinaswa na mtambo wa
radar katika eneo hilo sio kweli.
Amesema
mawasiliano ya mwisho ya ndege hiyo iliyokuwa ikitoka Kuala Lumpur
kuelekea Beijing yalinaswa katika rasi iliyoko kati ya Malaysia na
Vietnam.
Ndege
na meli kadhaa zimekuwa zikitafuta mabaki ya ndege hiyo katika eneo la
bahari ya Malaysia, lakini hazijafanikiwa kupata mabaki ya ndege hiyo.
Msako unaendelea
Jeshi
la Malaysia limesema kuwa, mtambo wake wa radar unaashiria ndege hiyo
iliyotoweka, ilielekea eneo la Magharibi, mbali na njia iliyostahili
kupita kabla ya kutoweka.
Ndege hiyo MH370 ilitoweka siku ya Jumamosi, baada ya kupaa ikiwa na abiria mia mbili na thelathini tisa.
Juhudi za kimataifa za kutafuta ndege hiyo zimepanuliwa na kuimarishwa.
Awali
ilibainika kuwa watu wawili waliokuwa wakisafiri kwa kutumia paspoti
zilizoibiwa walikuwa raia wa Iran ambao hawana uhusiano na kundi lolote
la Kigaidi.

Ndege ya Malaysia iliyotoweka kabla ya kutoweka siku ya Jumamosi.Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment