Bern, Uswisi. Wakongwe wa soka, Zinedine Zidane na Ronaldo kwa
mara nyingine tena wamewakusanya wachezaji nyota mbalimbali wa zamani na
kucheza mechi kwa ajili ya kukusanya fedha kusaidia maskini.
Huu ni mwaka wa 11 nyota hao wanafanya hivyo.
Fedha zilizopatikana kwenye mechi iliyochezwa juzi
baina ya wachezaji hao nyota wa zamani na Young Boys ya Uswisi kwenye
uwanja wa taifa wa Bern nchini Uswisi zitapelekwa kusaidia watu
waliokumbwa na kimbunga Haiyan nchini Phillipines.
Katika mechi hiyo wachezaji nyota wa zamani waliichapa Young Boys mabao 8-6.
Wachezaji wa kikosi cha nyota hao wa zamani
walioshiriki katika mechi hiyo ni makipa Carlo Cudicini (Italia) na
Antonios Nikopolidis (Ugiriki).
Mabeki ni Paolo Maldini, Fabio Cannavaro, Gianluca
Zambrotta (Italia), Fernando Hierro, Michel Salgado (Hispania), Jamie
Carragher (England), Paulo Ferreira, Fernando Couto (Ureno).
Viungo ni Zinedine Zidane, Patrick Vieira, Robert
Pires, Christian Kerembeu (Ufaransa), Luis Figo, Paulo Sousa (Ureno),
Pavel Nedved (Jamhuri ya Czech ), Freddie Ljungberg (Sweden), Gaizka
Mendieta (Hispania), Gennaro Gattuso (Itali), Ronald de Boer (Uholanzi),
Santiago Solari (Argentina), Hidetoshi Nakata (Japan) na Steve
McManaman (England).
Washambuliaji ni Ronaldo, Marta, Giovane Elber
(Brazil), Davor Suker (Croatia), Hakan Sukur (Uturuki), Youri Djorkaeff
(Ufaransa), Christian Vieri (Italia) na Nuno Gomes (Ureno).
No comments:
Post a Comment