Iringa. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala
jijini Dar es Salaam, Jerry Silaa amewataka wananchi wa Jimbo la Kalenga
kumchagua mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia CCM, Godfrey Mgimwa kwa
kuwa serikali iliyopo madarakani imeundwa na CCM.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara wa kumnadi
mgombea wa CCM, Silaa alisema hawana budi kuichagua CCM kwa sababu ndiyo
iliyoshika dola kwa miaka mitano 2010-2015.
Alisema kama wananchi wa kijiji hicho na jimbo kwa
ujumla wanataka maendeleo ya haraka, lazima waiunge mkono CCM kwa
kumchagua Godfrey Mgimwa.
“Wananchi wa Kijiji cha Mgama na jimbo lote, kama
mnataka maendeleo kwa haraka ni lazima muichague CCM na siyo chama
kingine kwa sababu Serikali iliyopo madarakani ni ya CCM,” alisema
Silaa.
Naye mwenyekiti wa CCM Tawi la Ihemi, Greyson
Mlowe alimtaka mgombea ubunge katika jimbo hilo kutatua changamoto ya
maji katika kata ambapo wabunge waliopita walijaribu kuitatua bila ya
mafanikio.
Alisema yeye ni mzaliwa wa Kata ya Mgama kwa muda
mrefu , kuna baadhi ya viongozi wamekwenda kuomba kura, lakini
walipopata walipotea na kuwaacha wakihangaika na changamoto zao.
Naye Mgimwa alisema atashirikiana na viongozi wa
nyanja mbalimbali kuhakikisha anatatua changamoto za wananchi wa jimbo
hilo endapo watamchagua.
Alisema kuwa kutokana na changamoto nyingi za
wananchi hao, ameamua kutumia elimu aliyonayo ili aweze kuzifikisha kwa
viongozi mbalimbali na kupatiwa ufumbuzi.
Uchaguzi huo utafanyika Jumapili ijayo.
CHANZO MWANANCHI
CHANZO MWANANCHI
No comments:
Post a Comment