Wednesday, 5 March 2014

kura za siri zazua mukundi bungeni

Macho na masikio ya Watanzania kwa sasa yapo  Dodoma ambako mjadala ya maandalizi ya mchakato wa kuandika Katiba Mpya.
Kwa karibu wiki sasa, hoja inayojadiliwa na wajumbe wa Bunge hilo maalumu la katiba ni kanuni zitakazotumika kuongoza chombo hicho.
Mjadala wa kuwepo kwa kura ya siri  au ya wazi katika kufanya uamuzi, umeonekana kuzua makundi mawili, moja likijitanabaisha kama kundi la wazalendo na linalotetea masilahi ya jamii huku jingine likitazamwa kuwa linatetea masilahi ya chama tawala.
Hata hivyo, wachambuzi wa masuala ya kisiasa nchini wanaona kuwa kuwapo kwa makundi yenye misimamo, hakuna madhara katika mchakato unaoendelea.
Badala yake wanaeleza kuwa makundi hayo yamesababishwa na misimamo ya wale waliowatuma kuwawakilisha.
Wachambuzi hao wanasema kwa kuwa wajumbe wa Bunge hilo wanayawakilisha makundi yenye mitazamo, mahitaji na mawazo tofauti na ndiyo maana haishangazi kuona kutofautiana kwa mawazo na hata kuonekana kuwepo kwa makundi yenye misimamo na mawazo tofauti.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Alexander Makuliko anasema mvutano unaoonekana kuendelea mjini Dodoma ni wa kawaida na uliotarajiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ukweli kuwa wajumbe hao ni wawakilishi wa makundi mbalimbali na yenye misimamo tofauti katika jamii.
Anasema kutokana na ukweli huo, haishangazi kukitokea kinachoonekana kuwa misimamo ya baadhi ya makundi kwa kuwa misimamo ile ni maelekezo na makubaliano ya makundi wanayoyawakilisha.
“Hili la baadhi ya wajumbe kuonekana kutetea au kuwa na misimamo ya makundi fulani ni la kawaida na lilitarajiwa kabisa.Kumbuka kuwa makundi lazima yapeleke hoja zake, yavutane na lenye hoja nzuri ndiyo lisikilizwa,” anasema.
Hata hivyo, Dk. Makulilo anapingana na dhana kuwa masilahi ya taifa yawekwe mbele na kuhoji unawezaje kuyapima masilahi ya taifa bila kuyaweka hayo makundi mbalimbali ya jamii?
“Kule kuna wawakilishi wa makundi mbalimbali, wapo wawakilishi wa wavuvi, wakulima, wafugaji na wale wanaotoka katika vyama vya siasa, yote haya ni makundi na kila moja lina masilahi yake…hivyo, hakuna ubaya hata kidogo inapotokea kila moja likahakikisha kuwa kundi lake linafaidika na katiba inayoandaliwa

{chanzo   mwananchi}

No comments:

Post a Comment