Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco amewaambia
wenzake kama wamedhamilia kutwaa ubingwa msimu huu ni lazima wahakikishe
wanaishinda Simba Jumapili na Mbeya City.
Bocco aliiambia Mwananchi kuwa hakuna kingine
zaidi ya kuwashinda wakongwe hao ili kuzidi kuwapoteza Yanga wanaokabana
nao jino kwa jino katika mbio hizo za ubingwa.
Mshambuliaji huyo alisema hawana budi kukomaa na
kuhakikisha wanashinda mechi hizo ili kuzidi kufufua matumaini yao ya
kupata ubingwa kwa mara ya kwanza msimu huu.
Alisema mechi walizobakiwa nazo ni ngumu ingawa
wengi wanaona kuwa watapata vikwazo zaidi katika mechi dhidi ya Simba na
Mbeya City hivyo wanataka kuwadhihirishia watu kuwa wamejipanga na
watavuka vikwazo vyote hivyo wanavyofikiria.
“Lengo letu msimu huu ni kutwaa ubingwa na ndio
maana tumejipanga na hatutaki kupoteza mchezo wowote, lakini muhimu
kwanza ni kukivuka hiki kigingi dhidi ya Simba Jumapili, iwe isiwe
lazima tujitahidi.
“Sasa hivi hatupaswi kupoteza mchezo wowote kwani
tukiteleza tu wapinzani wetu watachukua nafasi, maana hali ilivyo
tunakwenda kila mmoja anamuombea mwenzake apoteze ndio maana nawaomba
wenzangu tujitahidi tukomae mpaka mwisho,” alisema Bocco.
<MWANANCHI>
<MWANANCHI>
No comments:
Post a Comment