KATIKA tukio linalohusishwa na ushirikina, mwanamke mmoja
aliyejulikana kwa jina la Doto Omari (30, pichani) ameunguzwa na moto wa
ajabu sehemu zake za siri.
Tukio hilo la aina yake lilitokea alfajiri ya Machi 16 mwaka huu,
Mwananyamala – Kichangani, Dar, wakati mwanamke huyo alipokwenda chooni
kujisaidia.
Akizungumza na waandishi wetu, Doto alisema alipoanza kujisaidia,
alishangaa kuona moto mkubwa ukitokea ndani ya shimo la choo na
kumuunguza sehemu zake za siri, jambo lililomfanya apige kelele kuomba
msaada.
“Yaani ule moto ulikuwa mkubwa halafu wa kijani huku ukiwa na
muungurumo wa ajabu. Mimi nilishangaa kuuona ukinifuata na kuniunguza,”
alisema.
Kaka wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Adam, alisema
aliposikia kelele za moto, alikimbilia maji akijua ni wa kawaida.
“Mpaka sasa tumechanganyikiwa sana, hilo siyo tukio la kwanza, yako
mengi, nilishawahi kumuona mtu wa ajabu kainama kwenye mlango wa
kuingilia chooni halafu kufumba na kufumbua akapotea, hii nyumba siyo
kabisa.
“Wengi ukiwaambia jambo hili huona kama hadithi, lakini matukio ya
aina hii hapa Kichangani ni jambo la kawaida sema watu wanaogopa
kusema,” alisema Adam.AUo zaidi ya kumuona wifiye akigaragara
chini akidai kuungua.
Hadi waandishi wetu wanaondoka eneo la tukio, ndugu hao walikuwa
wakijiandaa kumpeleka Doto kwa mganga wa kienyeji maeneo ya Lugoba,
Chalinze kwa matibabu
chanzo GPL
No comments:
Post a Comment