Wednesday, 12 March 2014

TAMBWE: NIKO TAYARI KUJIUNGA NA YANGA


MSHAMBULIAJI wa kimataifa ya Simba kutoka Burundi, Amissi Tambwe, amesema atakuwa tayari kujiunga na Yanga endapo tu klabu hiyo itakubali kumpa mshahara kama anaochukua mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa  Yanga inamhitaji mshambuliaji huyo ambaye anaongoza kwa kuzifumania nyavu katika michuano ya Ligi Kuu Bara ili kuimarisha safu yake ya…

Mshambiliaji  wa kimataifa ya Simba kutoka Burundi, Amissi Tambwe.
Na Sweetbert Lukonge
MSHAMBULIAJI wa kimataifa ya Simba kutoka Burundi, Amissi Tambwe, amesema atakuwa tayari kujiunga na Yanga endapo tu klabu hiyo itakubali kumpa mshahara kama anaochukua mshambuliaji Emmanuel Okwi.
Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa  Yanga inamhitaji mshambuliaji huyo ambaye anaongoza kwa kuzifumania nyavu katika michuano ya Ligi Kuu Bara ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.
Tambwe ambaye mshahara wake Simba ni Sh 1,275,000,  mpaka sasa ameshazifumania nyavu mara 19, akifuatiwa na Kipre Tchetche wa Azam ambaye ana mabao 10.
Akizungumza na Championi Jumatano, Tambwe alisema kuwa, kama kweli Yanga wanamtaka ni vyema wakazungumza kwanza na uongozi wa Simba, kisha wamfuate yeye.
Alisema endapo Simba itakubali kumwachia ajiunge na Yanga ambayo Jumapili iliyopita ilitupwa nje ya michuano ya kimataifa na Al Ahly ya Misri, basi atahitaji mshahara kama anaopewa Okwi hivi sasa.
“Mwenyewe kiwango changu unakijua, hivyo unadhani ni mshahara gani mzuri ambao Yanga wanaweza kunipa? Haina ubishi nitawaomba wanilipe kama anavyolipwa Okwi.
“Hata hivyo kama kweli wananihitaji ningeomba waanze kwanza kuzungumza na viongozi wangu kwa sababu bado nina mkataba na Simba na wakifikia makubaliano ndipo waje kwangu tuzungumze ila mshahara nitataka kama wa Okwi,” alisema Tambwe.
Okwi ambaye alijunga na Yanga hivi karibuni akitokea SC Villa ya Uganda na usajili wake ukazua utata mkubwa hapa nchini, analipwa zaidi ya Sh milioni 6.5 kwa mwezi.
Tambwe kwa sasa anaongoza kwa ufungaji wa mabao kwenye Ligi Kuu ya Tanzania Bara akiwa ana mabao 19 huku ligi timu yake ya Simba ikiwa imebakiza michezo mitano ligi imalizike.
Chanzo global publisher

No comments:

Post a Comment