Dar es Salaam. Kocha wa Mabingwa wa Soka Afrika, Al Ahly,
Mohamed Youssef amesema kati ya wachezaji anaowatilia shaka na ana hofu
nao katika mechi ya marudiano Jumapili itakayochezwa saa mbili kamili
kwa saa za hapa nchini ni Mrisho Ngasa, Hamis Kiiza na Didier Kavumbagu.
Youssef alikaririwa na mtandao wa mmoja wa Misri,
akisema kuwa wachezaji hao ni tishio kwake kwa mchezo huo, lakini
akamtaja mshambuliaji mwingine, Emmanuel Okwi kuwa ni kati ya wachezaji
hatari kwa ngome yake.
“Kutokana na wachezaji wetu kuwa majeruhi,
imesababisha kushindwa mechi tatu zikiwemo za ligi,” alisema Youssef na
kudai kuwa wachezaji wake watakuwa na kazi ya kumchunga, Mrisho Ngasa
ambaye alionyesha soka ya kiwango cha juu.
Ngasa, ambaye hakufanya vizuri kwenye majaribio
yake 2009 katika klabu ya England ya West Ham, alifunga mabao matatu
katika kila mechi dhidi ya Komorizone katika mechi za hatua ya awali.
Yanga ilipambana na Al Ahly katika mchezo wa
kwanza wa raundi ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita na Yanga
kushinda bao 1-0 lililofungwa na Nadir Haroub ‘Canavaro’ baada ya
kuunganisha mpira wa kona uliompita kipa wa Al Ahly, Sherif Ekrami na
kujaa wavuni.
Tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),
limeandika barua Fifa kuomba maelekezo iwapo mashabiki wa Yanga
wataruhusiwa kushuhudia pambano hilo ambalo Yanga inatakiwa kucheza kufa
aukupona kuhakikisha inatoka na ushindi ili iweze kusonga mbele kwenye
michuano hiyo.
“Wasiwasi wetu Fifa isije ikairuhusu Yanga
ikajikuta haina mashabiki, tunategemea mpaka leo jioni (jana) tutakuwa
tumeshafahamu msimamo wa Fifa kama wanaruhusu mashabiki wa Yanga nao
waende, na pia wasije wakaenda wakajikuta wanabaki nje ya uwanja,”
alisema Wambura. {chanzo mwananchi}
No comments:
Post a Comment