Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila
akimlalamikia Mwenyekiti wa muda wa Bunge hilo kwa kutompa nafasi ya
kuchangia bungeni mjini Dodoma jana. Picha na Silvan Kiwale
Dodoma. Wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakipitisha Rasimu ya Kanuni za kuendesha Bunge hilo, suala la aina ya kura kwa ajili ya kuamua masuala mbalimbali, limekwama na litaamuliwa na wabunge baada ya kuanza kwa vikao rasmi vya Bunge hilo.
Dodoma. Wakati wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakipitisha Rasimu ya Kanuni za kuendesha Bunge hilo, suala la aina ya kura kwa ajili ya kuamua masuala mbalimbali, limekwama na litaamuliwa na wabunge baada ya kuanza kwa vikao rasmi vya Bunge hilo.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo kwa mvutano wa
takriban wiki nne kuhusu rasimu, hasa kifungu cha 37 na 38 kinachoeleza
aina ya kura kati ya wazi na ya siri.
Hata hivyo, wajumbe wawili wa Bunge hilo,
Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Felix Mkosamali wa NCCR- Mageuzi
walisusia kupitisha azimio la kukubali Kanuni za Bunge hilo, wakidai
kusalitiwa katika uamuzi huo na wenzao walioko kwenye Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Wajumbe na viongozi mbalimbali wa vyama vyenye
ushawishi bungeni, kwa pamoja waliridhia na kulegeza misimamo yao ili
upatikane mwafaka wa kutengeneza Katiba Mpya ndani ya wakati.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti ndani na nje ya
Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, viongozi hao walisema masilahi ya
Watanzania katika mchakato wa Katiba ni ya muhimu kuliko masilahi
binafsi ya makundi.
Kinana asema
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Abdulrahaman
Kinana alisema pamoja na malumbano makali yanayoendelea katika Bunge la
Katiba, anaamini sasa Katiba itapatikana.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti
hili jana mjini Dodoma, Kinana alisema haoni tatizo katika malumbano
hayo na kwamba anaamini yanatokana na mitazamo tofauti ya makundi
wanayotoka wajumbe.
“Pale kila kundi lina msimamo wake, iwe Chadema,
CUF, NCCR-Mageuzi, CCM na hata makundi katika kundi la wateule wa Rais.
Ilikuwa ni lazima kushuhudia mivutano ya aina hiyo,” alisema Kinana na
kuendelea: “Lakini mwisho wa yote, nawaasa wajumbe kuwa na moyo wa
kuvumiliana kwa sababu lazima kila kundi litetee hoja zake kulingana na
tathmini yake juu ya mwenendo wa siasa na matarajio yake ya baadaye.”
Alisema kwa msingi huo, haoni tatizo kwa CCM
kuweka misimamo katika baadhi ya hoja, ingawa chama hicho pia hakitasita
kulinganisha nguvu ya hoja zake na hoja za wengine.
Mtikila, Mkosamali wasusia
Mchungaji Christopher Mtikila na Felix Mkosamali
ndiyo wajumbe pekee waliosusia kupitisha azimio la kukubali kanuni za
Bunge hilo, wakidai kusalitiwa na wenzao walioko kwenye Umoja wa Katiba
ya Wananchi (Ukawa).
{mwananchi}
{mwananchi}
No comments:
Post a Comment