Wananchi wa Kijiji cha Ndiwili mkoani Iringa wakishangilia helikopta
iliyombeba mgombea ubunge Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya Chadema, Grace
Tendega wakati ilipokuwa ikiondoka. Chadema ilifanya kampeni za uchaguzi
mdogo kijijini hapo, juzi.
Wananchi wengi wajitokeza katika mkutano wa kampeni jimboni Kalenga, huku wengi wao wakiishangaa helikopta ya Chadema.
Chopa ya Chadema ilifika katika kijiji hicho saa sita mchana na kufanya mbwembwe kwenye anga la kijiji hicho kabla ya kutua.
Baada ya kutua na wajumbe kupanda jukwaani,
viongozi hao waliwashambulia viongozi wa CCM kwa madai kuwa wameanza
kuliingiza taifa kwenye mfumo wa kifalme, baada ya kujiwekea utamaduni
wa kurithishana madaraka. Akizungumza katika mkutano huo Lema
alisema:“Taifa linaelekea kubaya tulipokwenda, na hii inatokana na CCM
kuanza mfumo wa kurithishana madaraka,” alisema.
Lema aliwataka wakazi wa Kalenga kuupinga mfumo
huo kwa vitendo na kwa kuanza ni vyema wakampigia kura mgombea ubunge
kupitia Chadema Grace Tendega.
Naye Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji
Peter Msigwa alimshambulia Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philp Mangula
akidai ni mmoja wa viongozi wasio wakweli kwa wananchi.
Alisema kiongozi huyo aliwadanganya wananchi kuwa
chama chake kingewaengue viongozi wote walioingia kwenye nafasi zao kwa
rushwa katika kipindi cha miezi sita na hakuna kichofanyika.
“Kama aliwadanya wananchi kuwa angechukua hatua za
kuwatimua viongozi wa CCM walioingia kwenye nafasi zao kwa rushwa ndani
ya kipindi cha miezi sita na hadi leo hilo halijatekelezeka,atawezaje
kuasaidia ninyi wananchi wa Kalenga?alihoji Msigwa na kuongeza;
“Ninaomba msikubali kudanganywa na viongozi hawa
alipochaguliwa na kuingia kushika wadhifa w aKaimu mwenyekiti bara
alisema anarejesha maadili ndani ya CCM na kwamba angewavua magamba wote
walioingia kwenye nafasi zao kwa rushwa ndani ya kipindi cha miezi
sita…hadi leo hawajachukua hatua,leo wanawaambia watatekeleza ahadi
walizoziahidi zipi walikuw awapi siku zote”alisema.
Msigwa aliwataka wakazi wa Kalenga kutafanya
makasa kuchagua CCM kwakuwa viongozi wake hawana dhamira ya kweli ya
kuwaaidia wananchi kupiga hatua za maendeleo.{CHANZO MWANANCHI}
No comments:
Post a Comment