David Silinde, alisema kwa uzoefu wa Bunge la Jamhuri kundi la
wachache huchukuliwa kama wapinzani na kupewa muda mchache ambao
hautoshelezi kuwasilisha taarifa yao.
Alisema maoni ya wachache kwenye Bunge hilo si lazima yatokane na
upinzani, bali kutoka kwenye makundi mbalimbali yanayounda Bunge hilo,
hivyo ni vyema wakapewa muda wa dakika 50.
Mjumbe Lucas Malunde, alisema isijengeke dhana kuwa kundi la wengi
ndilo lenye hoja za msingi na wachache wanaotoka upinzani hoja zao haina
msingi, kuna muhimu wa kuongezewa muda na kuwasilisha taarifa yao na
kujadiliwa.
Mjumbe Julius Mtatiro alisema dunia ya sasa ni demokrasia kwa
wachache kupewa nafasi kwa kuwa wanaweza kuwa na mawazo mazuri kuliko
walio wengi.
Mjumbe wa kamati ya Kanuni na Kumshauri Mwenyekiti, Evod Mmanda,
alisema muda wa saa moja kwa taarifa ya wengi unatosheleza na nusu saa
kwa wachache unatosheleza.
"Hisia zinajengeka kuwa hoja ya wachache unaweza kupigwa, kamati inaweza kuja na hoja ya wengi na ikapigwa vile vile," alisema.
Aidha, mjumbe Halima Mdee, alisema anashangazwa na uamuzi wa
Mwenyekiti wa muda, Pandu Ameir Kificho, kuruhusu maboresho mengine
kutoka kwa wajumbe na kusahau kuwa kifungu cha 33 kilishajadiliwa na
kutolewa uamuzi wa saa moja kwa taarifa ya wengi na nusu saa kwa taarifa
ya wachache.
Hata hivyo, Bunge hilo ilipitisha kanuni hiyo kwa maboresho ya
taarifa ya wachache kusomwa kwa nusu saa na ya wengi kusomwa na
Mwenyekiti wa kamati kwa saa moja.
CHANZO:
NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment