Dar es Salaam. Wakati Polisi Morogoro ikiwa ya kwanza kupanda
Ligi Kuu msimu wa 2014/2015, timu nyingine tano za ligi daraja la kwanza
zinachuana kuwania nafasi mbili zilizobakia.
Timu hizo ni Kanembwa JKT, Mwadui na Stendi United
ambazo zinachuana kusaka nafasi moja ya kucheza Kigi Kuu kwenye kundi
C, ambapo kila moja ina pointi 19 na mechi nne mkononi.
Katika kundi A, timu ya African Lyon iliyoshuka
daraja msimu uliopita inachuana vikali na Ndanda kuwania nafasi moja
katika kundi A ya kucheza Ligi Kuu msimu ujao.
Kwa mujibu wa ofisa wa bodi ya ligi (TPLB), Joel
Balisidya, Lyon inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi 23 ikifuatiwa na
Ndanda yenye pointi 22 huku kila moja ikibakiwa na michezo miwili.
“Kundi B tayari Polisi Morogoro imepanda kucheza Ligi Kuu ikiwa na
pointi 25 na mechi mbili mkononi ambazo timu nyingine za kundi lake
haiwezi kuzifikisha,” alisema Balisidya.
Katika kundi hilo la B, Mlale JKT ina pointi 17
sawa na Bukina Faso na Lipuli huku kila moja ikiwa na michezo miwili
ambayo hata zikishinda michezo yote zitafikisha pointi 23 kila moja.
Kwenye kundi C, Toto African ina wakati mgumu wa
kupanda Ligi Kuu mbele ya Kanembwa JKT, Mwadui na Stendi United ambazo
zinachuana kutafuta tiketi hiyo moja.
Chanzo mwananchili
Chanzo mwananchili
No comments:
Post a Comment