Waziri
Mkuu wa Malaysia Najib Razak akitangaza leo juu ya utafiti wa rada
kuonyesha kuwa ndege iliyopotea imeangukia katika bahari ya Hindi.
Tangazo
hilo limetolewa wakati ndege ya majini ya Australia ikiwa njiani
kuelekea kunakoonekana vitu hivyo vilivyoonwa na ndege za kijeshi wakati
wa msako wake.
Wanajeshi wa jeshi la Australia wakiwa ndani ya ndege katika kituo cha Kijeshi cha AP-3C Orion.Ndege hiyo ya abiria ya Malaysia iliyokuwa na namba MH370 ilitoweka katika rada za kiraia saa moja baada ya kuruka kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing ikiwa na watu 239 ndani yake hapo Machi 8 mwaka huu.
Hakuna habari zilizothibitishwa juu ya kuonekana kwa mabaki ya ndege hiyo, ingawa kumekuwa na vitu vinavyoonekana huko pwani ya Australia vinavyodhaniwa huenda ni sehemu ya chombo hicho. Ndugu wa abiria waliokuwemo ndani, wameanza mipango ya kusafiri kuelekea huko.
Hata hivyo, vitu vilivyoonekana kwenye
satellite ya China na Ufaransa, bado havijaweza kufikiwa na kutambuliwa
kama vina uhusiano wowote na ndege hiyo ambayo ni gumzo kwa sasa
duniani.
CHANZO NI DAILYMAILY

No comments:
Post a Comment