London, England. Leicester City ilitoka nyuma
kwa mabao 3-1 na kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Manchester
United katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana.
United walionekana kama wangeibuka na ushindi
wakati Robin van Persie alipofunga bao la mapema kabla ya Angel Di Maria
kufunga la pili, lakini bao la kichwa la Leonardo Ulloa lilifanya
matokeo kuwa 2-1 kabla ya Ander Herrera kufunga la tatu kwa United.
Leicester walirudi uwanjani kwa kasi na kupata
penalti iliyofungwa na David Nugent na Esteban Cambiasso alisawazisha
bao la tatu, wakati Jamie Vardy akifunga la nne kabla ya Ulloa kufunga
la tano.
Ikiwatumia washambuliaji watatu, Radamel Falcao,
Wayne Rooney na Robin van Persie, United ilishindwa kucheza vizuri
katika kipindi cha pili na kuiruhusu Leicister kumiliki mpira
walivyotaka.
Bao la Andre Schurrle la kipindi cha pili
lilisawazishwa na Frank Lampard na kufanya mchezo kati ya Manchester
City na Chelsea kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Vijana wa kocha Jose Mourinho walilazimisha sare
hiyo ugenini katika Uwanja wa Etihad na kufikisha pointi 13 kileleni
ikiwa na michezo mitano iliyocheza.
Katika mchezo huo, beki wa pembeni wa City, Pablo
Zabaleta alitolewa kwa kadi ya pili ya njano kutokana na kumchezea
vibaya Diego Costa kipindi cha pili.
Mchezo huo ulionyesha kuwa ungekuwa na kadi
nyekundu baada ya wachezaji saba kuonyeshwa kadi za njano katika kipindi
cha kwanza. Kwa matokeo hayo, Chelsea imeendelea kubaki kileleni mwa
msimamo ikiwa na tofauti ya pointi tatu, ikifuatiwa na Southamptom wenye
pointi 10.
No comments:
Post a Comment