Monday, 22 September 2014

SIMBA KAKABWA KOO NA WAGOSI WA KAYA


0
Share

Dar es Salaam. Makosa ya mabeki wa Simba yaliyofanywa dakika za majeruhi, yaliipa sare ya kwanza msimu huu baada ya kufungana 2-2 na Coastal Union ya Tanga katika mechi ya kupendeza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana.Katika mchezo huo, Coastal walitumia dakika nane za majeruhi kipindi cha pili kufunga bao la kusawazisha na kuinyima Simba ushindi katika mechi yao ya kwanza msimu huu.Bao la Coastal lilitokana na makosa ya kiufundi ya mabeki wa Simba walioshindwa kuweka ukuta imara kuzuia kiki ya adhabu ndogo iliyopigwa na Ramadhan Salum dakika ya 82 na kwenda moja kwa moja kwenye kamba za Wekundu hao.
Kosa la kwanza lililoigharimu Simba na kuipa Coastal kupata bao la kwanza, lilifanywa na kiungo Pierre Kwizera aliyeshindwa kuumiliki vizuri mpira kabla ya kunaswa na wachezaji wa Coastal Union na Lutimba Yayo Kato kuutumbukiza wavuni kwa kiki ya karibu na lango.
Kwa matokeo ya mchezo wa jana, Simba na Coastal Union zimezoa pointi moja kila mmoja.
Mchezo wa jana uliokamilisha mechi za kwanza za raundi ya kwanza ya ligi hiyo, ulianza kwa Simba kusalimia lango la wapinzani wao na kuandika bao la kwanza kupitia kwa Shaaban Kisiga. Kisiga alifunga bao hilo kwa mpira wa faulo dakika ya saba kabla ya Amis Tambwe kufumania nyavu dakika ya 36 akiunganisha kwa kichwa akimalizia krosi ya Emmanuel Okwi.
Kwa upande mwingine, juhudi za Simba kupata mabao, zilichangiwa kwa kiasi kikubwa na Okwi kwani bao la kwanza, aliangushwa nje ya 18 na beki wa Coastal, Tumba Swedi kabla ya Kisiga kufunga kwa faulo, pia alipiga krosi ambayo iliunganishwa na Tambwe kuandikia bao la pili.Jitihada za Union kusaka bao zilizaa matunda katika dakika ya 67 baada ya Lutimba Yayo Kato kufanikiwa kumtungua kipa wa Simba, Ivo Mapunda kufuatia pande la Itubu.
Ikishambulia mfululizo, Coastal Union ilisawazisha dakika ya 82 kupitia kwa Ramadhan Salum aliyetandika mpira wa faulo uliokwenda moja kwa moja nyavuni.
Simba waliianza mechi ya jana kwa kasi huku wakitawala sehemu ya kiungo, lakini mipira yao ya mwisho haikuwa makini na hivyo kushindwa kutengeneza nafasi za mabao huku Haruna Chanongo akipoteza chache walizozipata.
Katika kipindi cha kwanza, Coastal walitumia muda mwingi kulinda lango zaidi kuliko kushambulia, huku pia ikifanya mashabulizi ya kushtukiza wakimtumia mshambuliaji Itubu Imbem.
Kipindi cha pili, Simba walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Chanongo na Tambwe na nafasi zao kuchukuliwa na Uhuru Selemani na Rafael Kiongera, wakati Coastal waliwatoa Seleman Kibuta, Razak Khalfan na Joseph Mahindi na nafasi zao kuchukuliwa na Lutimba Yayo Kato, Ayoub Yahaya na Abbas Athuman.
Mabadiliko hayo yaliwanufaisha Coastal kwani walipata mabao mawili. Akizungumza baada ya mechi kumalizika kocha wa Simba, Patrick Phiri alisema: “Coastal walicheza vizuri, sijafurahia matokeo tuliyoyapata ila tutajiandaa kwa ajili ya mechi ijayo.”

MAN U YABAMIZWA 5

V
London, England. Leicester City ilitoka nyuma kwa mabao 3-1 na kuibuka na ushindi wa mabao 5-3 dhidi ya Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa jana.
United walionekana kama wangeibuka na ushindi wakati Robin van Persie alipofunga bao la mapema kabla ya Angel Di Maria kufunga la pili, lakini bao la kichwa la Leonardo Ulloa lilifanya matokeo kuwa 2-1 kabla ya Ander Herrera kufunga la tatu kwa United.
Leicester walirudi uwanjani kwa kasi na kupata penalti iliyofungwa na David Nugent na Esteban Cambiasso alisawazisha bao la tatu, wakati Jamie Vardy akifunga la nne kabla ya Ulloa kufunga la tano.
Ikiwatumia washambuliaji watatu, Radamel Falcao, Wayne Rooney na Robin van Persie, United ilishindwa kucheza vizuri katika kipindi cha pili na kuiruhusu Leicister kumiliki mpira walivyotaka.
Bao la Andre Schurrle la kipindi cha pili lilisawazishwa na Frank Lampard na kufanya mchezo kati ya Manchester City na Chelsea kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Vijana wa kocha Jose Mourinho walilazimisha sare hiyo ugenini katika Uwanja wa Etihad na kufikisha pointi 13 kileleni ikiwa na michezo mitano iliyocheza.
Katika mchezo huo, beki wa pembeni wa City, Pablo Zabaleta alitolewa kwa kadi ya pili ya njano kutokana na kumchezea vibaya Diego Costa kipindi cha pili.
Mchezo huo ulionyesha kuwa ungekuwa na kadi nyekundu baada ya wachezaji saba kuonyeshwa kadi za njano katika kipindi cha kwanza. Kwa matokeo hayo, Chelsea imeendelea kubaki kileleni mwa msimamo ikiwa na tofauti ya pointi tatu, ikifuatiwa na Southamptom wenye pointi 10.

Monday, 8 September 2014

MWIGULU NCHEMBA AFANYA ZIARA JIMBONI KWAKE


Mh:Mwigulu Nchemba akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr.Kone wakati wakukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Maabara za  Kisasa Katika Shule za Jimbo la Iramba,Hapa ni Shule ya Kijiji cha Usule.Kufikia Tar.31/09/2014 Mkuu wa Mkoa anategemea Kumkabidhi Mh:Rais Jakaya Kikwete Maabara zote za Shule za Sekondari zikiwa zimekamilika ndani ya Mkoa wa SIngida kuendana na Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi.
 Mh:Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wananchi wa Kijiji cha Usule waliofika kusikiliza mambo mbalimbali ya Utekelezaji wa Shughuli za Maendeleo.Kwaya ya akina mama Kiji cha Usule wakitumbuiza mbele ya Mgeni Rasmi Mh:Mwigulu Nchemba(hayupo pichani).Vijana wakifurahia Ushindi wao katika Michuoano ya MWIGULU CUP,Hii ni timu ya Kijiji cha Usule.Akina mama wakionesha kadi zao za Chama cha Mapinduzi kuonesha kuwa wao bila CCM haiwezekani.Wananchi wakishangilia baada ya Kuona Nguzo za Umme zikipita kijijini kwao Ishara kuwa Umeme umewafikia.
Mh:Mwigulu akimsikiliza Mmoja wa Wazee wa kijiji cha Usule.Mkutano unaendelea huku Mh:Mwigulu nchemba akiwafafanulia mambo mbalimbali ya maendeleo wanakijiji wa Usule,Kubwa ni Usambazaji wa maji hapo Kijijini ambao tayari umekwisha anza,Pia amesisitiza Kusuka nyaya za Umeme wakati huu Umeme unapowekwa kwenye nguzo,Ukiingiza Umeme wakati huu mafundi wakiwa wanasambaza nyaya ni Bei nafuu 27000/= tu.Ilikukamilisha Ujenzi wa Maabara ya Shule ya Usule Mh:Mwigulu amechangia Mifuko 100 ya Sementi na ameagiza kwenye Upungufu wowote Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi atoe taarifa.Hivyo hivyo amesaidia Uchimbaji wa Bwawa la maji kama Mpango wa Muda mfupi wakati Bomba za Maji zikiendelea Kusambazwa kijiji chote cha Usule.Baadhi ya Vijaja Kijiji cha Kibaya wakiwa kwenye Jezi zao za MWIGULU CUP.Mh:Mwigulu Nchemba akikabidhi Mchango wake wa bati 70 kwa Diwani wa kata ya Mbelekesye kwaajili ya kuezeka Madarasa ya shule ya Mbelekesye yaliyoongezwa.Pia amechangia Mifuko 100 na Mbao kwaajili ya kupau madarasa hayo.
Wakati hili likifanyika katika kijiji cha Kibaya,Mh:Mwigulu Nchemba jana alikabidhi Mabati 320 kijiji cha Misuna kwaajili ya Ujenzi wa Zahanati.Wananchi wakibaya wakifurahia na Mbunge wao.

OKWI HURU KUCHEZA SIMBA

Wajumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya TFF wakiwa katika mkutano jijini Dar es Salaam jana. Picha na Said Khamis.      
Dar es Salaam. Utata wa Emmanuel Okwi umemalizwa rasmi na mchezaji huyo wa Uganda sasa yupo huru.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilikutana jana na kupitia masuala mbalimbali ikiwamo mgogoro wa kimkataba kati ya klabu ya Yanga na mchezaji Emmanuel Okwi.
Mkataba huo ulipitiwa na kamati ikiwamo kumsikiliza mchezaji mwenyewe pamoja na upande wa Yanga na kuridhika kuwa mkataba kati ya pande hizo umevunjika.
Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa mkataba wa pande mbili haupo kwa sababu Yanga ilikiuka kipengele namba 8 kuhusu malipo ya ada ya usajili.
“Yanga ikiwa mwajiri, haikutekeleza kipengele hicho cha kimkataba hadi kufikia Juni 27 mwaka huu ilipoandika barua TFF kuomba mkataba huo uvunjwe. Kwa maana hiyo Okwi ni mchezaji huru, hivyo yuko huru kujiunga na timu yoyote,” alisema Wambura.
Alifafanua kuwa mkataba ni uhusiano kati ya mwajiri (Yanga) na mwajiriwa (Okwi), ambapo Kamati imebaini kuwa uhusiano huo haupo, hivyo hakuna mazingira ya pande hizo mbili kuendelea kufanya kazi pamoja.
Pamoja na Yanga kuwasilisha pingamizi la kuwepo mmoja wa wajumbe katika kikao kwa sababu za kimaslahi (conflict of interests), walifahamishwa kuwa kilichopo mbele ya kamati ni mgogoro wa kimkataba kati ya Yanga na Okwi, na si usajili.
Pia lilijitokeza suala la Okwi kutakiwa na klabu ya Wadi Degla ya Misri.
Kamati imeiagiza Sekretarieti ya TFF kulifanyia uchunguzi suala hilo na kulitolea taarifa katika kikao kijacho.
Hata hivyo mjumbe ambaye Yanga ilimpinga hakushiriki katika kuchangia hoja na kutoa maamuzi.
Uamuzi wa kamati ulifanyika baada ya majadiliano, hivyo hakukuwa na suala la kupiga kura.
Kuhusu pingamizi la Coastal Union kwa Abdi Banda, Kamati imebaini kuwa klabu hiyo imevunja mkataba kati ya pande hizo mbili kwa kushindwa kumlipa mchezaji huyo mshahara wa miezi mitatu mfululizo kama takwa la mkataba.

ZITO :ATOA YA MOYONI


Dar es Salaam. Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ameeleza tofauti yake na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akisema imesababishwa na watu aliowaita wapambe.
Zitto (37), ambaye alikuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, alisema kuwa hata kuvuliwa nyadhifa zake ndani ya chama kulisababishwa na wapambe hao, lakini akasisitiza kuwa hana kinyongo tena kwa kuwa alishamwomba Mungu na sasa amesamehe kabisa.
Tofauti za wawili hao hazijawahi kutolewa hadharani licha ya mitandao mbalimbali kuzungumzia kuharibika kwa uhusiano wao ikinukuu habari kutoka vikao vya ndani vya Chadema.
Hata hivyo, mapema mwaka huu, Zitto alirushiwa tuhuma nzito na Chadema kutokana na uhusiano wake na baadhi ya makada wa CCM, lakini mbunge huyo aliyahusisha maneno hayo na mwenyekiti wake na aliandika maneno makali dhidi ya Mbowe kwenye ukurasa wake wa facebook.
Lakini katika mahojiano na Mwananchi yaliyofanyika wiki iliyopita nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam, Zitto alionekana kujutia kuharibika huko kwa uhusiano wao na kusema “wapambe ndiyo wanatugombanisha”.
“Sina shida yoyote na Mbowe, naamini ipo siku tutagundua wapambe walituathiri na ndiyo waliotufikisha hapa,” alisisitiza Zitto bila kutaja ni kina nani hasa.
Zitto alisema yeye na Mbowe wametoka mbali tangu akiwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na hafurahii uhusiano wao ukiishia katika hali hiyo.
“Naumia sana, lakini naamini ipo siku ama nikiwa hai au nimekufa watu wataujua ukweli,” alisema mwanasiasa huyo kijana aliyepata umaarufu kutokana na uwezo wake wa kujenga hoja.
Alisema, akiwa mwenyekiti wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo Kikuu (Daruso) yeye na mwenyekiti wake ndiyo waliokijenga chama wakati huo Mbowe akiwa mbunge wa Hai.
Alisema wakati huo Mbowe alikuwa akienda chumbani kwake kusuka mikakati ya kuiinua Chadema na kwamba walikuwa wakila chips pamoja na wakati mwingine kwenye klabu ya usiku ya Bilicanas inayomilikiwa na Mbowe.
“Wakati mwingine naangalia, naumia sana. Wakati tunafanya hayo yote wengine walikuwa CCM, wengine walikuwa wafanyabiashara, lakini sasa ndiyo wana sauti katika chama,” alisema Zitto.
Zitto alisema kuwa wakati huo walikuwa na kampeni yao waliyoiita ‘Real Madrid’ ambayo ilikuwa na lengo la kuingiza kila mwanasiasa bora katika chama chao.
****MWANANCHI***