Saturday, 6 December 2014

SIMBA INATISHA

SIMBA imefanya usajili mwingine wa kimyakimya baada ya kumsajili mshambuliaji raia wa Gambia.
Mshambuliaji huyo ametajwa kwa jina la Omar Mboob aliyewasili jana usiku kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
Ingawa viongozi wa Simba hawakuwa wakipokea simu jana, taarifa za uhakika zinaeleza mshambuliaji huyo kinda anatarajia kuanza mazoezi leo na Simba.
“Kweli Simba wamekuja usiku wa jana (juzi) wakampokea mchezaji mmoja na wamesema anatokea Gambia.
“Walikuja na Hiace yao hapa wakampokea na kuondoka naye lakini walifanya mambo yao harakaharaka utafikiri kuna jambo la uficho.“Nilimsikia kiongozi mmoja akitaka waondoke haraka hapa airport kwa kuwa waliwahofia Yanga,” kilieleza chanzo cha uhakika kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Simba alipoulizwa jana, alionekana kushangazwa na swali hilo, lakini hakutoa jibu.“Nani kakuambia, mimi sijui lolote. Wamekuambia anatokea nchi gani? Ila ukweli sina habari ndugu yangu,” alisema.
Ila taarifa za uhakika, zinasisitiza mshambuliaji huyo amefichwa na viongozi wa Simba wamekuwa wakifanya siri kubwa kuhakikisha haijulikani.
Lengo ni kuepuka Yanga au klabu nyingine kuingilia kati ili wajaribu kuona kiwango cha mchezaji huyo kutokea katika Jiji la Banjul, Gambia.Iwapo Mgambia huyo atafuzu, basi itakuwa ni hatari kwa Warundi, Amissi Tambwe na Pierre Kwizera kwa kuwa mmoja wao atalazimika kuachia nafasi.SI

No comments:

Post a Comment