Stori: ShowbizWAKATI siku zikizidi kukatika kuelekea Desemba 6, katika ule Usiku wa Nani Kama Mama ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar ambapo Mfalme wa Masauti, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuweka historia mpya ndani ya ukumbi huo.

Mfalme wa Masauti, Christian Bella ‘Obama’.
Akipiga stori na Showbiz, Meneja wa Bella, Amiri Marusu
aliongelea usiku huo ambao umekuwa gumzo kubwa kwakuwa ni mara ya kwanza
kufanyika uzinduzi wa Albamu ya Nani Kama Mama ndani ya Dar Live hivyo
Bella amejipanga vya kutosha kwa kuweka historia mpya ukumbini hapo.
“Mashabiki wakae mkao wa kusikia ngoma kali zote kama vile Hanitaki
Tena, Usilie aliyoimba na Banana Zoro, Msaliti, Nakuhitaji na nyingine
kibao ambazo zipo katika albamu hiyo,” alisema Amiri.
Christian Bella ‘Obama’ akipozi.
Bella ambaye alitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kutua
katika bendi ya Akudo Impact na kutengeneza ngoma kali kama Walimwengu
si Wanadamu, Bomoa Bomoa, Safari Sio Kifo, Yako Wapi Mapenzi na nyingine
nyingi. Ametokea kujizolea umaarufu kwa sauti nyingi tofauti kiasi cha
kupelekea kutungiwa jina la Mfalme wa Masauti.
No comments:
Post a Comment