Saturday, 6 December 2014

SIMBA INATISHA

SIMBA imefanya usajili mwingine wa kimyakimya baada ya kumsajili mshambuliaji raia wa Gambia.
Mshambuliaji huyo ametajwa kwa jina la Omar Mboob aliyewasili jana usiku kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.
Ingawa viongozi wa Simba hawakuwa wakipokea simu jana, taarifa za uhakika zinaeleza mshambuliaji huyo kinda anatarajia kuanza mazoezi leo na Simba.
“Kweli Simba wamekuja usiku wa jana (juzi) wakampokea mchezaji mmoja na wamesema anatokea Gambia.
“Walikuja na Hiace yao hapa wakampokea na kuondoka naye lakini walifanya mambo yao harakaharaka utafikiri kuna jambo la uficho.“Nilimsikia kiongozi mmoja akitaka waondoke haraka hapa airport kwa kuwa waliwahofia Yanga,” kilieleza chanzo cha uhakika kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.
Mmoja wa viongozi wa Kamati ya Utendaji ya Simba alipoulizwa jana, alionekana kushangazwa na swali hilo, lakini hakutoa jibu.“Nani kakuambia, mimi sijui lolote. Wamekuambia anatokea nchi gani? Ila ukweli sina habari ndugu yangu,” alisema.
Ila taarifa za uhakika, zinasisitiza mshambuliaji huyo amefichwa na viongozi wa Simba wamekuwa wakifanya siri kubwa kuhakikisha haijulikani.
Lengo ni kuepuka Yanga au klabu nyingine kuingilia kati ili wajaribu kuona kiwango cha mchezaji huyo kutokea katika Jiji la Banjul, Gambia.Iwapo Mgambia huyo atafuzu, basi itakuwa ni hatari kwa Warundi, Amissi Tambwe na Pierre Kwizera kwa kuwa mmoja wao atalazimika kuachia nafasi.SI

CHRISTIAN KUFUNIKA DAR

Stori: Showbiz
WAKATI siku zikizidi kukatika kuelekea Desemba 6, katika ule Usiku wa Nani Kama Mama ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem, jijini Dar ambapo Mfalme wa Masauti, Christian Bella ‘Obama’ anatarajiwa kuweka historia mpya ndani ya ukumbi huo.
Mfalme wa Masauti, Christian Bella ‘Obama’.
Akipiga stori na Showbiz, Meneja wa Bella, Amiri Marusu aliongelea usiku huo ambao umekuwa gumzo kubwa kwakuwa ni mara ya kwanza kufanyika uzinduzi wa Albamu ya Nani Kama Mama ndani ya Dar Live hivyo Bella amejipanga vya kutosha kwa kuweka historia mpya ukumbini hapo. “Mashabiki wakae mkao wa kusikia ngoma kali zote kama vile Hanitaki Tena, Usilie aliyoimba na Banana Zoro, Msaliti, Nakuhitaji na nyingine kibao ambazo zipo katika albamu hiyo,” alisema Amiri.
Christian Bella ‘Obama’ akipozi.
Bella ambaye alitokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kutua katika bendi ya Akudo Impact na kutengeneza ngoma kali kama Walimwengu si Wanadamu, Bomoa Bomoa, Safari Sio Kifo, Yako Wapi Mapenzi na nyingine nyingi. Ametokea kujizolea umaarufu kwa sauti nyingi tofauti kiasi cha kupelekea kutungiwa jina la Mfalme wa Masauti.