Saturday, 11 October 2014

JEMBE KINANA AENDELEA KUVUNJA CHADEMA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akionesha kadi 27 za wananchama wa Chadema  waliokihama chama hicho na kujiunga na CCM kaatika mkutano wa hadhara uliofanyika Mjini Nyololo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010. Kulia aliyevaa shati jeupe ni aliyekuwa Katibu wa Kata ya Igowole, Josephat Soda ambapo wengine ni miongoni mwa walio kuwa wafuasi wa Chadema.
 Aliyekuwa Katibu wa Chadema Kata ya Igowole, Joephat Soda akikabidhi bendera ya chama hicho kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya yeye na wenzie 26 kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM wakati wa mkutano huo.
 Kinana akimkabidhi kadi ya CCM, Josephat Soda baada ya kutanga kujiunga na CCM katika mkutano huo.
 Josephat Soda akielezea jinsi alivyoamua kuondoka Chadema na kujiunga na CCM, ambapo alisema amechoka na chama kilichosheheni uongo, ambapo viongozi wa Chadema alidai kuwa walitoa maagizo kuwaakope fedha za  kujengea Mnara wa mwandishi wa habari Marehemu David Mwangosi, aliyeuawa wakati wa vurugu za Chadema na Polisi katika Mji wa Nyololo, ambapo walimuahidi kumtumia fedha zilizotumika kujenga mnara huo ahadi ambayo hadi sasa haalipwa na anadaiwa na muuza simenti na muuza saruji alikokopa. CCM imeamua kulipa madeni yote aliyokuwa akidaiwa.
Wanachama wa CCM wakiwemo wapya kutoka Chadema, wakiapa kiapo cha utii cha CCM baada ya kukabidhiwa kadi wakati wa mkutano huo.
<<<<<<<<GPL>>>>>>>>

JAMBAZI SUGU LAUWAWA ARUSHA

 
Wakazi wa Jiji la Arusha wakiwa katika Kituo cha Polisi mkoani humo kushuhudia mwili wa mtu anayedaiwa kuwa jambazi sugu, Ramadhan Abdallah Jumanne (Rama Ndonga), aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi usiku wa kuamkia jana. Picha na Happy Lazaro.       


Arusha. Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kumuua jambazi aliyekuwa akiutikisa mkoa huo kwa matukio ya kuteka na kuwapora wanawake wenye magari na kisha kuwapiga risasi.
Mtu huyo aliyefahamika kwa kwa jina la Ramadhan Abdallah Jumanne maarufu kama Rama Ndonga (37) Mkazi wa Moivo hatimaye ameuawa polisi baada ya kupigwa risasi katika majibizano na askari wa jeshi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jambazi huyo aliuawa usiku wa kuamkia jana majira ya saa 2:04 usiku katika Kijiji cha Moivo, Kitongoji cha Enaboishu wilayani Arumeru.
Alisema baadhi ya matukio ya ujambazi aliyowahi kuhusika nayo ni lililotokea Agosti 6 mwaka huu saa 3:30 usiku maeneo ya Kwa Iddi ambapo walimpiga risasi sehemu ya shingo mwanamke Shamimu Rashid aliyekuwa Mkazi wa Sakini wakati akijiandaa kuingia nyumbani kwake na kumuua.
Kamanda Sabas alitaja tukio lingine ni la Agosti 21 mwaka huu majira ya saa 1:00 huko maeneo ya Olasiti, jambazi huyo akiwa na mwenzake kwenye pikipiki walimjeruhi kwa kumpiga risasi ya mdomoni na kutokea kichwani mtoto Christen Nickson mwenye umri wa miaka mitatu na nusu na kisha kufanikiwa kupora Sh200,000 na baadaye majeruhi huyo alifariki dunia akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Mount Meru.
Aidha, kukamatwa kwa jambazi huyo ni baada ya polisi kutumia mbinu za kisasa na kufika nyumbani kwa marehemu na polisi walimwamuru ajisalimishe lakini alikaidi na kuanza kuwarushia risasi hali iliyosababisha askari kujibu mapigo na hatimaye kusababisha kifo chake.
Alisema kuwa, baada ya upekuzi mwili wa marehemu ulipatikana na bastola aina ya Glock 19 yenye namba RLU 976 iliyotengenezwa nchini Australia ikiwa na magazine yenye risasi 14 ambayo alikuwa ameishika mkononi pamoja na maganda matano ya risasi.
Aidha, upekuzi zaidi uliofanywa katika chumba chake ulibaini magazine moja yenye risasi 15 na magazine mbili zenye uwezo wa kubeba risasi 30 kila moja, redio call moja yenye nembo ya ITSS/UNICTR, pikipiki aina ya Toyo Power King rangi nyekundu yenye namba za usajili T 507 BSU.
Upekuzi zaidi ulibaini kofia ngumu ya kuendesha pikipiki rangi nyekundu, plate number ya pikipiki yenye namba T 805 CVD, pingu moja, Glock Fab Defence moja na vifaa vya kusafishia bastola pamoja na koti jeusi.
Kamanda Sabas alisema polisi wanaendelea kumsaka mwenzake waliyekuwa wakitumia naye pikipiki hiyo, ili kuweza kuutokomeza mtandao huo ambao umekuwa tishio jijini Arusha.
Kutokana na tukio hilo, watu walifurika kituo cha polisi kushuhudia mwili wa marehemu ambaye aliutikisa mji huo.

POLICE 120 WATIMULIWA CHUONI MOSHI

 
Moshi. Maofisa wa Polisi wapatao 120 wa Jeshi la Polisi, waliokuwa wakihudhuria mafunzo ya kupandishwa vyeo katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi (MPA), wametimuliwa chuoni hapo.
Habari za uhakika zilizopatikana jana kutoka ndani ya chuo hicho zamani kikijulikana kama CCP, zimedai uamuzi wa kuwaondoa chuoni ulitangazwa jana na mkuu wa chuo hicho, Matanga Mbushi.
Vyanzo mbalimbali vililidokeza gazeti hili kuwa, waliotimuliwa chuoni hapo ni maofisa ambao wana ulemavu wa aina mbalimbali walioupata wakiwa wanatekeleza majukumu yao ya kazi.
Habari hizo zilisema hadi jana saa 9:00 alasiri, maofisa hao walikuwa ofisi za mkuu wa chuo hicho wakisubiri kupatiwa maelekezo ya namna ya kurejea katika vituo vyao vya kazi mikoa mbalimbali.
“Wako 120 hivi walikuja hapa (MPA) kwa ajili ya kuchukua kozi za Koplo, Sajenti, Meja na ‘Assistant Inspector’ (wakaguzi wasaidizi), lakini ndiyo hivyo wametuambia tuondoke,” kilidokeza chanzo chetu.
Hata hivyo, ofisa mmoja alilidokeza gazeti hili kwamba mkuu wa zamani Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, ambaye amestaafu, ndiye wa kulaumiwa kwa kutoheshimu mapendekezo ya wataalamu.
“Tulimwambia IGP Mwema kwamba ni vizuri kama maofisa wenye ulemavu kama baadhi ya vigezo wanavyo basi wapewe vyeo huko huko mikoani, lakini wasiende chuoni,” alidokeza na kuongeza;
“Tulipendekeza yafunguliwe madarasa ya kanda wakishafanya mtihani wa kawaida wapewe vyeo huko huko, lakini wakija chuoni ni lazima wahudhurie vipindi vyote ambavyo vinafanya chuo kiitwe chuo.
“Chuo chochote kile kina vigezo vyake na kwamba ili mtu apate cheo alichokwenda kukisomea ni lazima ahudhurie asimilia 95 ya vipindi ikiwamo kwata, medani za kivita na kuzuia vurugu,”alisema.
Chanzo kingine kililidokeza gazeti hili kuwa maofisa hao waliripoti chuoni hapo wiki mbili zilizopita na katika uchunguzi, walibainika wana ulemavu ambao hawawezi kumudu mafunzo ya ukakamavu.
Mmoja wa maofisa hao waliotimuliwa alilalamika kuwa kitendo hicho siyo cha kiungwana kwa kuwa ulemavu huo waliupata wakiwa kazini wakilitumikia Taifa na hawajashindwa kuingia darasani.
“Baadhi yetu tumefanya kazi miaka 20 wengine 25. Wamekatika miguu. Wako trafiki wamegongwa na polisi wengine wamepigwa risasi na majambazi wakapata ulemavu si sawa kutunyima vyeo,”