Tuesday, 29 April 2014

MASHABIKI WA CHELSEA NA LIVERPOOL WALIVYO PIGANA

Pata hiyo na ukome: Shabiki wa Liverpool akimchapa konde wa Chelsea nje ya Uwanja wa Anfield
VURUGU ilizotokea nje ya Uwanja wa Anfield kufuatia Liverpool kufungwa na Chelsea mabao 2-0 jana.
Picha zinaonyesha kitimutimu cha maana nje ya Uwanja wa Anfield Road baada ya mashabiki wa Liverpool kuwavaa mashabiki wa Chelsea waliokuwa wakiimba jina la Nahodha wa Wekundu hao, Steven Gerrard baada ya mechi.
Shabiki mmoja alitupa konde kwa mwenzake, wakati wengine walitenganishwa na Polisi.

Makosa ya Gerrard yalisababisha bao la kwanza la Chelsea lililofungwa na Demba Ba na mashabiki wa The Blues wakawatia hasira Liverpool kwa kuimba jina la mchezaji huyo. 
Mashabiki wa Chelsea wakizomea kwa jeuri ya ushindi wa 2-0
Mashabiki wakizipiga chanzo ni kuzomewa kwa Steven Gerrard
Polisi wakituliza ghasia
Baba akiongozana na kijana wake kutoka eneo la vurugu huku watu wakiendelea kuchapana nyuma yake
Polisi walilazimika kuwaachanisha watu wengine waliopelekana hadi chini katika mapambano yao
Polisi wakiwwka uzio baina ya mashabiki wa Liverpool na Chelsea
Mashabiki wa Liverpool wakisema na Polisi waliokuwa wakituliza ghasia hizo.
Credit:Matukio na Vijana

KINGUNGE AZUNGUMZA KUHUSU JAJI WARIOBA

Kwanza kabisa nimshukuru Mungu kwa kunipa uzima siku hii ya leo na nikaweza kuandika haya unayoyasoma.
Wiki iliyopita nilimsikiliza kwa makini sana mkongwe wa siasa nchini, mzee Kingunge Ngombale Mwiru alipokuwa akitoa mchango wake katika Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma.
Mzee Kingunge akisisitiza jambo
Kabla ya kusimama na kuongea, mzee Kingunge nilikuwa najiuliza ni nani wa kutuliza hiki anachofanyiwa Jaji Joseph Sinde Warioba kwa sababu alichokifanya siyo chake binafsi bali ni cha tume na yeye alikuwa ni kiongozi tu.
Haipendezi hata kidogo kuona mjumbe wa bunge anamuambia Jaji wa Warioba afunge mdomo! Hii si haki hata kidogo na siyoheshima.
Mzee Kingunge hakumung’unya maneno alisema wazi kuwa kumtukana au kumshambulia mzee huyo au wajumbe wa tume yake ni sawa na kukitukana Chama Cha Mapinduzi, bila shaka kada huyo alisema hivyo kwa sababu wajumbe wa tume ya kuratibu rasimu ya katiba waliteuliwa na mwenyekiti wa chama ambaye pia ni rais wa nchi.
Akaweka wazi kuwa hatakubali hata kidogo kuona wajumbe wa bunge maalum wakitumia misimamo ya vyama vyao kumshambulia Jaji Warioba au wajumbe wa tume aliyokuwa akiiongoza kwa sababu wanaomshambulia wanaonesha utovu mkubwa wa adabu kwa kuwa chama kina maadili na adabu katika kushughulikia mambo mbalimbali.
Wakati mzee Kingunge akisema hayo naye Jaji Warioba aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ameuliza maswali saba ya msingi kwa wajumbe wa Bunge la Katiba wanaopinga Rasimu ya Katiba waliyoikabidhi iliyotolewa na tume yake akitaka wawajibu wananchi ili kutuliza kiu yao.
Jaji Warioba ambaye tangu awasilishe Rasimu ya Katiba Desemba 30, mwaka jana amegeuka kuwa adui kwa watu wanaotaka muundo wa serikali mbili, aliuliza maswali hayo katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti wa Taasisi ya Twaweza kuhusu mchakato wa Katiba ambapo alisema:
“Kwanza, jibuni kwa nini mnapinga muundo wa muungano wakati walioupendekeza ni wananchi? Sheria inasema uwepo muungano na mapendekezo katika rasimu hayasemi muungano usiwepo.
Kumbukeni kuwa wananchi walitakiwa kutoa mapendekezo ya namna ya kuuboresha.”Katika swali lake la pili, Warioba alisema kwa nini Tanganyika imevaa koti la muungano? Kwa kuwa katika ukusanyaji wa maoni wananchi walieleza kuwa Serikali ya Muungano wa Tanzania ya sasa siyo ya muungano, ni ya Tanganyika.
Katika swali la tatu alisema wajumbe hao wanatakiwa kujibu maelezo ya wananchi ambao waliieleza tume hiyo kuwa katiba imevunjwa na madaraka ya rais yamechukuliwa na sasa kuna marais wawili katika nchi moja.
“Tume inapewa lawama kubwa, wajibuni wananchi hii tume ilitumwa na nani kukusanya maoni ya wananchi? Waambieni ilikusanya maoni hayo kwa kutumia sheria ipi zaidi ya ile ya Mabadiliko ya Katiba?” alisema Jaji Warioba katika swali lake la nne.
Katika swali lake la tano, Warioba aliwataka wajumbe hao kutoa sababu za kumtuhumu kuwa amependekeza muundo wa serikali tatu kwa sababu yeye pamoja na Joseph Butiku walikuwa wajumbe wa Tume ya Jaji Kisanga na Jaji Nyalali ambazo nazo zilipendekeza muundo wa serikali tatu, kitu ambacho alisema si kweli na hawakuwahi kuwa mjumbe wa tume hizo.
Pia, aliwataka wajumbe hao kujibu swali la sita, kwa nini hawataki kuzungumzia yaliyomo katika Rasimu ya Katiba na badalayake wanageuza rasimu hiyo kuwa imeandikwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Katika swali lake la saba, aliwataka wajumbe kujibu kwa nini wanaishutumu Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuwa imeingiza maoni yake, wakati ilikusanya maoni hayo kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba?
Nilisikiliza kwa makini mijadala ndani ya bunge na kugundua kuwa badala ya kujadili hoja za msingi,
wajumbe wa bunge hilo walikuwa wakitoa lugha za kejeli na matusi kwa baadhi ya watu, kitendo ambacho kwangu mimi naona si sahihi na kinaweza kuligawa taifa kwa sababu yaliyomo katika Rasimu ya Katiba yametokana na maoni ya baadhi ya wananchi.
Siamini kabisa kuwa wajumbe wa tume alijitungia kile kilichoandikwa kwenye rasimu. Siyo hoja hata kidogo kutaja mabaya ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Wajumbe wote wa Bunge Maalum la Katiba watafakari na kuboresha rasimu na kamwe wasitumie nafasi yao kujadili watu. Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Monday, 28 April 2014

JINSI MAGEREZA WANAVYOPAMBANA NA WAFINGWA WAKOROFI

'Wafungwa' wakijifua kupambana na askari Magereza katika moja ya maonesho yaliyotia fora sana kwenye sherehe za miaka 50 ya Muungano katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo
Askari akipambana na 'Mahabusu' aliyeasi
Askari akila sahani moja na 'wafungwa' watatu
Askari anapangua teke....
Kisha anakata zote bee....
Mfungwa hoi...
Anadakwa kilaaiiini....
Hii ilikuwa ni igizo tu, kwani hakukuwepo na mfungwa halisi bali askari waliovalia aina ya nguo za wafungwa....Chanzo Michuzi Blog

UKAWA KUSIMAMISHA MGOMBEA MMOJA URAISI 2015

Dar es Salaam. Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeanza maandalizi ya kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, gazeti hili limebaini.
Kadhalika, vyama hivyo ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi na CUF vinakusudia kuwa na mgombea mmoja wa nafasi za wabunge na madiwani, ikiwa ni hatua ya kuzikabili nguvu za chama tawala, CCM.
Habari zilizolifikia gazeti hili zinasema tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo wamekubaliana kuanza mchakato huo na wameandika mapendekezo na kuyapeleka katika sekretarieti za vyama vyao kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi.
Chanzo chetu kilidokeza kuwa kamati ya wataalamu kutoka vyama hivyo tayari imeundwa ili kuandaa taratibu zitakazotumika katika kufanikisha mkakati huo.
Wenyeviti wa vyama hivyo walipoulizwa kwa nyakati tofauti kuhusu mpango huo hawakukubali moja kwa moja, badala yake walisema ni mapema mno kuzungumzia suala hilo katika vyombo vya habari.
Ukawa ni umoja ambao uliviunganisha vyama vyenye malengo yanayofanana katika Bunge Maalumu la Katiba na vimekuwa vikishinikiza kuzingatiwa kwa mapendekezo ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba hususan muundo wa Muungano wenye serikali tatu, tofauti na serikali mbili za sasa.
Umoja huo pia uliwaongoza wajumbe wa Bunge Maalumu ambao ni wanachama wake kutoka nje kususia mchakato wa Katiba Mpya kutokana na kile walichodai kuwa ni kutokuridhishwa na jinsi mambo yanavyokwenda.
Taarifa za kuwapo kwa mpango wa kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu ujao, zimekuja siku chache tangu kufichuliwa kwa mpango mwingine wa kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri kivuli ambalo litawajumuisha wabunge wa vyama hivyo katika Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
Baraza la kivuli la sasa linawajumuisha wabunge kutoka Chadema pekee, ambacho kinaunda Kambi Rasmi ya Upinzani bungeni tangu kuanza kwa Bunge la 10, Novemba 2010.
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema atapanga upya baraza lake katika siku za mwanzo za Bunge la Bajeti, linalotarajiwa kuanza Mei 6, mwaka huu mpango ambao umeungwa mkono na wenyeviti wa CUF na NCCR Mageuzi.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alisema uamuzi huo ni hatua kubwa katika ushirikiano na kwamba tayari alikwishawaarifu wabunge wa chama chake wawe tayari kushiriki katika baraza hilo.

<<<<<MWANANCHI>>>>>>>

DIAMOND MARUFUKU KUKANYAGA CHINA


STAA  wa  muziki  wa  bongo  fleva  nchini, Abdul  Nassib  "Diamond"  ametakiwa  kutokanyaga  kabisa  nchini  China  na  kwamba  akitokeza  pua  yake  nchini  humo  asahau  kabisa  kurudi  uraiani...

Hiyo  inafuatia  kijana  mmoja  mtanzania  kukamatwa  wiki  iliyopita  uwanja  wa  ndege  wa   Macau   China  na  kudai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....

Habari  kutoka  Macau  China  zinadai  kuwa  kijana  huyo  aliyejulikana  kwa  jina  moja  la  Manyota  alikamatwa  akiwa  kwenye  harakati  za  kuingiza   mzigo  huo  wa  dawa  za  kulevya  kwa  kupitia  uwanja  wa  ndege  wa  Macau....

Kwa  mujibu  wa  vyanzo  vyetu  vya  habari, inaarifiwa  kuwa  Manyota  alikamatwa  Alhamisi  ya  wiki  iliyopita  katika  uwanja  uleule  aliokamatwa  mtanzania  mwingine  Jackline  Patrick, anayesotea  rumande  mpaka  hii  leo  huko  huko  Macau  China.....

Kijana  mmoja  wa  kitanzania  anayefanya  shughuli  zake  huko  China  amedai  kuwa  Manyota  alikamatwa  na  maofisa  wa  usalama  wa  uwanja  wa  ndege  na  katika  utetezi  wake  alidai  kuwa  yeye  ni  mwanamuziki  toka  Afrika  Mashariki...

Mtanzania  huyo  aliendelea  kudai  kuwa, Manyota  baada  ya  kukamatwa  alianza  kubabaika  kwa  kujifanya  mwanamuziki  na  baadae  akadai  kuwa  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania....

"Alijifanya  yeye  ni  mwanamuziki, baadae  akabadilika  na  kudai  yeye  ni  mcheza  shoo  wa  mwanamuziki  Diamond  kutoka  Tanzania  na  kwamba  ndani  ya  ule  mzigo  alikuwa  hajui  kuna nini  zaidi  ya  kuombwa  na  jamaa  zake  wa  Dar  awapelekee  nchini  China"...Alisema  mtanzania  huyo

Inasemekana  kuwa, ili  kujiridhisha, maofisa  hao  wa  usalama  wa  uwanja wa  ndege    walimtaka  kijana  huyo  aoneshe  moja  ya  kazi  zake  na  yeye  akaishia  kuwaonesha  moja  ya  video  za  Diamond  kupitia  mtandaoni  na  kumuonesha  mmoja  wa  wacheza  shoo  wa  mwanamuziki  huyo  kuwa  ndo  yeye  Manyota...

Inasemekana  kuwa, pamoja  na  utetezi  wake  huo  ambao  unaweza  kumuingiza  matatani  Diamond,maofisa  hao  wa  usalama  walishndwa  kumuelewa  na  kumtupa  ndani.....

Mtanzania  huyo  alihitimisha  kwa  kudai  kuwa, kutokana  na  mazingira  yalivyo,ni  vyema  mwanamuzi  Diamond  akawa  makini   sana  kama  atakuwa  na  safari  za  kwenda  China  kwani  kwa  namna  moja  ama  nyingine  jina  lake  limewekwa  kwenye  orodha  ya  majina  machafu   na  wanaweza  kumkamata  kwa  lengo  la  kuujua  ukweli...

NIPO TAYARI KUFA KWA AJILI YA DIAMOND

Stori: Imelda Mtema
DADA wa hiyari wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Halima Kimwana amejichora tatuu ya jina la staa huyo na kudai anampenda na yupo tayari kufa kwa ajili yake.

Alisema ukaribu wake ni wa kawaida lakini yupo tayari kufa badala yake (Diamond).
“Nipo tayari kufa kwa ajili ya Diamond, nimechora tatuu ya jina lake mkononi kuonesha msisitizo, namkubali” alisema Halima.

DALILI ZA MWISHO WA DUN IA

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel & Bible Fellowship (FGBF) lenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, Zakaria Kakobe ameibuka na kuweka wazi kuwa kuonekana kwa Mwezi Mwekundu (Blood Moon),   Aprili 15, mwaka huu ni ishara kuu ya mwisho wa dunia kama maandiko yanavyosema katika Matendo 2:17-21, Uwazi linakumegea kwa kina.
Askofu Kakobe aliyasema hayo juzi kufuatia tukio hilo lililojiri siku tano kabla ya Sikukuu ya Pasaka ambapo mwezi wote ulipatwa (lunar eclipse) na kuwa mwekundu kama damu,  tukio ambalo pia litatokea tena mwakani.Kufuatia tukio hilo lenye kuogofya,…
NA WAANDISHI WETU
ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Full Gospel & Bible Fellowship (FGBF) lenye makao makuu yake jijini Dar es Salaam, Zakaria Kakobe ameibuka na kuweka wazi kuwa kuonekana kwa Mwezi Mwekundu (Blood Moon),   Aprili 15, mwaka huu ni ishara kuu ya mwisho wa dunia kama maandiko yanavyosema katika Matendo 2:17-21, Uwazi linakumegea kwa kina.
Askofu Kakobe aliyasema hayo juzi kufuatia tukio hilo lililojiri siku tano kabla ya Sikukuu ya Pasaka ambapo mwezi wote ulipatwa (lunar eclipse) na kuwa mwekundu kama damu,  tukio ambalo pia litatokea tena mwakani.Kufuatia tukio hilo lenye kuogofya, baadhi ya mitandao ya kijamii duniani kote imekumbushia maneno ya manabii mbalimbali lakini zaidi kutoka kwenye Biblia wakisema mwisho wa dunia sasa ni dhahiri.
MSIKIE KWA UNDANI
“Kinachotakiwa kwa watu sasa ni kuacha maovu na kumrudia Mungu. Ni wajibu wa kila mtu kujiweka tayari kwa kuokoka kwani bila kufanya hivyo watakaokutwa katika dhambi watatupwa jehanamu,” alitahadharisha  Askofu Kakobe.
Aliongeza kuwa, dalili zote za mwisho wa dunia zilizotajwa katika Biblia ziko wazi kwa sasa, kama vile hilo la mwezi wa damu, kuzuka kwa manabii wa uongo, vita ya nchi na nchi na ukoo kwa ukoo lakini akasema  hajui ni kwa nini watu hawataki kuokoka.
NAYE MAMA RWAKATARE
Naye Mchugaji wa Kanisa la Assemblies of God ‘Mikocheni B’ la jijini Dar, Mama Getrude Rwakatare alikiri kulijua hilo la mwezi kuwa wa damu na kusema katiba Biblia, Luka  21:25 Mungu amefafanua kuwa kuna dalili mbalimbali zitajitokeza siku za mwisho wa dunia na sasa zinaanza kuonekana, akawataka watu kuomba bila kuchoka.
“Dalili nyingine ni mataifa kupigana, upendo wa wengi kupoa, manabii wa uongo kuibuka na kadhalika. Haya tunayaona sasa, hivyo watu wote tumrudie Mungu,” alisema Mama Rwakatare.
NABII SUGUYE PIA
Uwazi lilibahatika kuzungumza na Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la Huduma na Neno la Upatanisho ambaye alisema dalili za mwisho wa dunia ni nyingi ambazo ni mataifa kupigana, kukosa uhusiano mzuri na kuzuka kwa manabii  wa uongo.
NABII GEODAVIE AJUAVYO YEYE
Uwazi lilikwenda mbele zaidi kwa kuzungumza na kiongozi wa Kanisa  la Ngurumo za Upako lenye makao makuu jijini Arusha, George David ‘GeoDavie’ ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Suala la kupatwa  kwa  mwezi  na kuwa  damu  ni ishara ya mwisho wa dunia lakini nasisitiza kuwa pia ni jambo la kisayansi zaidi.”
Alizidi kusema kuwa kilichoandikwa kwenye Biblia, Luka  21:25 (Tena kutakuwa na ishara katika jua na mwezi na nyota na katika nchi, dhiki ya mataifa wakishangaa kwa uvumi wa bahari na msukosuko wake) lazima kikubalike na kila anayemwamini Mungu.
IMANI MWAKYOMA WA TAG
Mchungaji Imani  Mwakyoma wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Magomeni jijini Dar, yeye alisema kupatwa kwa mwezi na kuonekana wa rangi ya damu ni mafundisho ambayo watumishi wa Mungu wamekuwa wakiihubiri kila kukicha.
“Tumekuwa  tukihubiri kwa muda wa miaka kumi sasa kwamba mwisho utafika pale tu ishara ya anga itakapoanza kuonekana, mwezi kuwa wa damu na jua kuwa giza, siku hizi kila mara jua linapatwa na kuwa giza, bado nini sasa hapo? Watu wamrejee Mungu,” alisema Mchungaji Mwakyoma.
ASKOFU MALASUSA, KARDINALI PENGO
Baadhi ya waumini wa kanisa la Romani Katoliki linaloongozwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo na Kanisa la KKT linaloongozwa na Askofu Dr. Alex Gerhaz Malasusa, walisema watumishi hao wa Mungu mara kwa mara wamekuwa wakihubiri watu kutubu kwa kuwa siku za mwisho wa dunia zipo dhahiri kwa sasa.

MCHUNGAJI WA MAREKANI
Naye John Hagee, Mchungaji wa Kanisa la Cornerstone, San Antonio, Texas Marekani na mwanzilishi wa muunganiko wa Wakristo nchini Israeli alishawahi kutoa kitabu akiongozwa na taasisi ya uchunguzi wa anga za juu ya nchi hiyo, NASA kwa kufanya makadirio kupitia historia ambapo aliandika uhusiano wa moja kwa moja kati ya kupatwa kwa mwezi na kuwa mwekundu na utabiri wa Waisrael na wanadamu wote.
NI KARIBU NA PASAKA TU?
Katika kitabu hicho, Mchungaji Hagee aliandika kwamba, zaidi ya miaka 500 iliyopita kupatwa kwa mwezi wa damu kulitokea siku ya kwanza ya Sikukuu ya Pasaka mara tatu tofauti.'
Hata Aprili mwaka huu, mwezi huo ulipatwa na kuwa mwekundu kuelekea Sikukuu ya Pasaka na itatokea tena mwakani kipindi cha Pasaka.
LAZIMA WATU WAJUE ISHARA
Mchungaji Hagee alifafanua kwamba kupatwa kwa mwezi ni lazima watu, hasa Wakristo waelewe ishara hizo.  Alisema katika Biblia, Joel: 2 na Matendo ya Mitume: 2 vyote vimeandika tukio hilo kwamba ndiyo mapito ya dunia kuelekea mwisho wake.
BAADA YA MATUKIO HAYA
Kwa mujibu wa Markell, mchambuzi wa mambo ya sayansi, kupatwa kwa mwezi na kuwa wa damu kutatokea tena katika mpangilio wa Oktoba 8, 2014, Aprili 4, 2015 na Septemba 28, 2015!
IMANI YA KIKRISTO
Hata hivyo, Markell anasema kuwa Wakristo wengi wanaamini maneno ya kale kwamba kupatwa kwa mwezi ni dalili ya ujio wa pili wa Kristo na hivyo kusababisha hofu miongoni mwa wale ambao hawajui maana halisi japo maelezo ya kisayansi yanafafanua jambo hili.
Alisema kimsingi, rangi ya mwezi ni nyekundu ambayo ipo katika anga ya dunia na kama dunia haina anga, moja kwa moja mwezi utafunikwa na giza.
Markell ambaye anaamini kwamba shetani yupo nyuma ya harakati za maendeleo, anasema hakuna mtu anayejua ishara za mwezi lakini alipendekeza kuwa dunia inapaswa kubashiri kwa habari mbaya.

<<<<GPL>>>>

Tuesday, 22 April 2014

CHADEMA YAENDELEA KUSAMBARATIKA

Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia Jiji la Mbeya Lucas Mwampiki




Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia Jiji la Mbeya Lucas Mwampiki amejiuzuru wadhifa huo kuanzia Aprili mwaka huu kutokana na mkanganyiko wa uongozi ndani ya chama hicho.

Mwapiki amesema amechoshwa na marumbano ya mara kwa mara na meza kuu ndani ya chama hicho katika ngazi ya wilaya hivyo kudhoofisha juhudi zake za kukijenga chama hicho.

Aidha Mwampiki amesema viongozi wa chama hicho wamekuwa na marumbano ya mara kwa mara hivyo yeye kama kiongozi hayupo tayari kuona mambo yanavurugika katika chama hicho.

Hata hivyo katika uamuzi aliouchukua Lucas Mwapiki amesema kuwa yeye atabakia kuwa mwanachama wa chama hicho na Diwani wa Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya.

Amewataka wanachama wamuelewe hivyo ameona yeye akae pembeni badala ya kuwa na muda mwingi wa kujadili migogoro ambayo haina tija na kuleta mkanganyiko kwa wanachama.

LIGI YA WILAYA YA MKINGA YAPAMBA MOTO

 Mkuu wa wilaya ya mkinga wakwanza mbele akikagua timu ya shikashika kasbla ya ligi ya walaya kuanza wa pili ni afisa tarafa wa tarafa ya mkinga na watatu ni mdhamini  wa ligi hiyo ndugu Saidi Mbaruku


Kikosi cha SHIKASHIKA FC  kabla ya mechi ya ligi ya wilaya ya mkinga


Kocha Mkuu wa SHIKASHIKA FC ndugu ALEX MWANGA "FERGASON" akitoa maelekezo kwa wachezaji wake kabla ya mechi ya ligi ya wilaya mkinga

Mkuu wa wilaya wakiendelea kufuatilia mechi hiya kati ya SHIKASHIKA FC NA CHUI FC hatimaye mechi hiyo iliisha chui fc 2 ,shikashika 1